NAFASI ZA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 282 540 674
Barua pepe: info@elct-elvd.org
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza, Geita na kwingineko.
Taarifa kuhusu Compassion International Tanzania: Ni shirika lililojikita katika kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwatoa watoto katika umaskini wa kiroho, kiuchumi na kimwili. Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria inatoa huduma ya mtoto kwa kushirikiana na Mshirika Mwenza Compassion International Tanzania (CIT) katika vituo vinne. Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:
NAFASI YA KAZI: Mratibu wa Elimu na Afya (Tangazo Limerudiwa)
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu KKKT-DMZV
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Huduma za Jamii
WAJIBU WA KAZI:
· Kuandaa na kuratibisha vikao vya kikatiba vya vitengo vya Elimu na Afya katika Dayosisi
· Kubuni njia za uendeshaji wa shule ya Sekondari ya Kilutheri Mwanza na Malya
· Kushauri uongozi juu ya uendeshaji miradi na program za vitengo vya Elimu na Afya
· Kusaidia na kuratibisha usajili wa shule za awali na sekondari DMZV
· Kuratibisha uanzishaji au ufufuaji wa shule za awali au msingi katika sharika
· Kusimamia utekelezaji wa sera na miongozo mbalimbali ya Elimu na Afya na kuhakikisha kuwa sera na miongozo inasambazwa kwa wadau
· Kuratibisha utoaji wa ushauri wa Afya kwa wakristo katika sharika za DMZV na kufuatilia uendeshaji wa vituo vya Afya
· Kuratibisha mradi wa huduma ya mtoto na kijana (compassion) unaotekelezwa katika sharika za DMZV
· Kubuni na kuandaa miradi ya Elimu na Afya katika Dayosisi
· Kusimamia watumishi katika vitengo vya Elimu na Afya katika Dayosisi
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Uzoefu katika kazi za huduma za jamii kama vile, Mahusiano ya Umma, Elimu ya Jamii, Uchunguzi wa Afya/Utabibu na maeneo mengine yanayohusiana na maeneo tajwa
· Uzoefu usipungua mwaka mmoja (1) katika nafasi ya uongozi katika taasisi za Elimu/Afya
· Uwezo katika kushughulikia masuala ya afya ya umma
· Mkristo (Mlutheri) na mwenye moyo wa kutumika kanisani
· Uwezo mzuri wa kuandaa ripoti
· Ujuzi na uelewa wa kanuni na misingi ya usimamizi wa program za Elimu na Afya
· Ujuzi wa kutumia kompyuta
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.
SIFA ZA KIELIMU:
· Shahada/Stashahada katika fani ya Afya ya Umma, Utabibu, Utawala wa Afya (Degree in Health Administration) au fani zingine zinazohusiana katika chuo kinachotambulika na serikali.
v NAFASI YA KAZI: Social Worker
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: KKKT- Usharika wa Sayuni Bugando
ATARIPOTI KWA: Mchungaji Kiongozi wa Usharika
WAJIBU WA KAZI:
· Kufanya mpangilio kwa kufuata mahudhurio ya ushiriki wa watoto/vijana kwenye program zote za kituo cha huduma ya mtoto.
· Kuhakikisha kuwa kila mtoto/kijana aliyefadhiliwa anaandikiwa barua kwa mfadhili wake kama ilivyopangwa
· Kutunza taarifa kamili, kwa wakati na sahihi ya mtoto kwa kulingana na mahitaji ya ofisi ya huduma ya Compassion
· Kufuatilia hali kwa ujumla na maendeleo ya watoto majumbani mwao mara zinapohitajika
· Kuandaa ripoti ya kazi ya kazi kila wiki na kila mwezi na kuiwasilisha kwa maratibu wa huduma ya mtoto
· Kuwajibika katika matokeo ya mtoto na viashiria vya kijamii kwa mujibu wa PFM
· Kuwatia moyo wazazi na walezi wa watoto na wajumbe wa kanisa kuwasaidia watoto kukua kiroho na kuwa na maendeleo mazuri katika masomo.
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Uwezo mzuri wa kutumia kompyuta na kuwa karibu na watoto muda wote
· Mkristo na mwenye moyo wa kutumika kanisani na kuwapenda watoto
· Uzoefu usiopungua angalau mwaka mmoja (1) katika fani ya maendeleo ya jamii.
· Mchapakazi mbunifu na mwenye uwezo wa kufanya kazi katika mazingira magumu na kupenda ushirika.
· Uwezo mzuri wa kuandaa ripoti
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.
SIFA ZA KIELIMU:
· Shahada ya kwanza ya maendeleo ya jamii, mahusiano ya Umma au elimu inayohusiana na maeneo hayo katika chuo kinachotambulika na serikali
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa wawasilishe Barua za maombi ya kazi, Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 07/08/2023
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 27/08/2023 SAA: 08:00 Mchana
NB: Maombi yawasilishwe kwa njia ya barua pepe tu. Na sio vinginevyo
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.