ZIARA YA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA DAYOSISI KATIKA SHAMBA LA MALYA

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA DAYOSISI (DMZV) WAFANYA ZIARA SHAMBA LA MALYA. Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Kanisa KKKT -Dayosisi Mashariki ya ziwa Victoria(DMZV) wamefanya ziara katika shamba linalomilikiwa na Dayosisi lililopo Malya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza . Halmashauri kuu ambayo ipo kwenye vikao vyake vya kikatiba January 08-2026 walitembelea shamba Hilo lenye ukubwa wa Ekari 1046 ili kujionea miradi mbalimbali inayofanyika katika shamba Hilo . Miradi Inayofanyika kwenye Shamba Hilo ni kilimo Cha mazao mbalimbali , mbogamboga ,Matunda ,ufugaji wa Nguruwe,mradi wa kufyatua tofali pamoja na ujenzi wa Shule ya secondary Yenye majengo 7,madarasa manne (4), Utawala,Maabara 3, Maktaba ,Hostel ya wakike na wakiume na ujenzi bado unaendelea ambapo wajumbe wakiongozwa na Askofu wa DMZV Oscar Lema wameshuhudia miradi hiyo. Baada ya kushuhudia miradi hiyo wajumbe wamepongeza maendeleo ya sasa ya shamba Hilo na kuuomba uongozi wa Dayosisi uendelee kulisimamia vyema ili liweze kuleta maendeleo kwa Dayosisi huku wakiwaomba wakristo wote wa DMZV Kuendelea kuunga mkono juhudi za Dayosisi kusimamia na kuendeleza miradi iliyopo ndani ya shamba Hilo