UZINDUZI WA JUKWAA LA UWAKILI INTERFAITH WAFANYIKA JIJI MWANZA 02/05/2024

Mkuu Wa Kanisa La KKKT Tanzania Askofu Doctor Alex Malasusa Ametoa Wito Kwa Viongozi Wa Dini Na Madhehebu Mbalimbali Kuwa Mstari Wa Mbele Kuhamasisha Utunzaji Wa Mazingira Ili Kujenga Jamii Itakayozingatia Mazingira Safi Na Afya Salama Muda Wote Askofu Malasusa Ameyasema Hayo Jijini Mwanza Wakati Wa Uzinduzi Wa Jukwaa La Uwakili Interfaith Lilioandaliwa Na Shirika La Danmission Ambapo Amesisitiza Kuwa Watu Waache Kukata Miti Hovyo Kwa Maana Watu Wengine Wanajitaidi Kupanda Miti Na Wengine Wanakata Miti Hovyo Hivyo Ni Lazima Viongozi Wa Kiroho Na Dini Wawe Mstari Wa Mbele Kwenye jitihada za Utunzaji Wa Mazingira Kwa Upande Wake Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu Wa Rais Muungano Na Mazingira Khamis Hamza Khamis amesema malengo ya serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 jamii iwe inatumia nishati safi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni yanayotajwa kuchangia uharibifu wa mazingira Naye Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza,Said Mtanda Amebainisha Mikakati ya mkoa haswa katika utunzaji wa mazingira aianisha utayari wa Kupanda Miti Milioni 23 Katika Kipindi Cha 2023-2026 Lakini Sasa Tayari Miti Milioni Saba Imepandwa Ofisa Program Wa Shirika La Danmission, Dickson Shekivuli Amesema Shirika Lao Litaendelea Kuhamasisha Jamii Utunzaji Wa Mazingira Huku Kaimu Katibu Mkuu Wa Kanisa La KKKT Rogath Mollel Akisema Ushirikiano Wa Dini Zote Ni Moja Ya Chachu Ya Mafanikio Ya Mradi Huo Kwani Utaunganisha Dini Zote na Kuhamasisha Upandaji Miti Uzinduzi Huo Uliohudhuriwa Na Viongozi Wa Din zote Kutoka Mikoa Ya Kanda Ya Ziwa Umeambatana Na Zoezi La Upandaji Miti Mitatu Uliyopandwa Katika Msikiti Wa Pasiansi Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.