UZINDUZI RASMI MRADI WA USHIRIKIANO WA UTUNZAJI MAZINGIRA

Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria amezindua rasmi mradi wa Ushirikiano wa Utunzaji wa Mazingira mtaa wa Penueli Nampalahala wilayani Bukombe Mkoani Geita Ijumaa tarehe 26/01/2024. Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria inatekeleza mradi huu kwa ushirikiano wa karibu na chama cha Misioni ZMO kutoka Ujerumani. Mradi huu unatekelezwa katika Sharika saba (7) za Dayosisi ambazo ni: Kaanani - Kiseke, Kaanani - Bupandwa, Nansio - Ukerewe, Imani Kanisa Kuu, Angaza - Igoma, Galilaya - Malya, Penueli Nampalahala na Chuo cha Biblia Nyakato-Mwanza. Katika tukio la uzinduzi viongozi wa serikali (AFISA MALIASILI na AFISA MISITU) wa Wilaya wa Bukombe wameshiriki vyema. Pia viongozi wamepongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira. KAULI MBIU: "Tuwe Mawakili Wema katika Utunzaji wa Mazingira". (Mwanzo 2:15) #Tunza Mazingira Yakutunze.