SHILLINGI MILLION 88 ZAHITAJIKA KUKAMILISHA MITA 391 ZA FENSI YA MWANZA LUTHERAN SECONDARY SCHOOL. Ujenzi wa fensi ya shule ya sekondari ya Mwanza Lutheran iliyopo mabatini jijini Mwanza umefikia asilimia 70 Huku zaidi ya million 88 zikihitajika ili kukamilisha Fensi hiyo Akisoma Taarifa ya ujenzi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa fensi hiyo Mwenyekiti wa Idara ya Mipango na Uwekezaji DMZV Bi. Alice Moses amesema ujenzi wa fensi hiyo yenye urefu wa Mita 973 umefikia kiwango kizuri kilichobaki ni kumalizia eneo la mita 391 lakini ukosefu wa fedha umefanya ujenzi huo kushindwa kukamilika kwa wakati . Akizindua fensi hiyo Jumapili ya March 01-2026 Askofu wa DMZV Oscar Itael Lema ameipongeza kamati hiyo na washarika wa DMZV kwa kutoa sadaka zao shilingi Miillion 91 ambazo zimejenga Mita 582 za Fensi hiyo kwani hakuna Fedha yoyote iliyotoka kwa Wafadhili Askofu Lema anaamini kuwa ujenzi wa Fensi hiyo utamalizika kwa nguvu ya washarika wa DMZV na kuwaomba walio ahidi michango wakamilishe mapema na ambao hawajaahidi Mungu awaongoze waweze kumtolea Mungu sadaka ya ujenzi wa fensi hiyoi ili watoto wasome kwenye mazingira salama zaidi . Aidha Askofu Lema amewasihi washarika wa KKKT-DMZV wasichoke kutoa michango kwaajili ya maendeleo ya Dayosisi kwani hakuna mtu mwingine wa kuijenga Dayosisi, huku akiwataka makatibu na wenyeviti wa miradi wa Sharika zote kuhakikisha wanaipa kipaumbele michango ya Dayosisi Kukamilika kwa ujenzi wa Fensi hiyo ambao utagharimu shilingi million 179 utasaidia kuongeza idadi ya wanafunzi kwenye shule hiyo ambayo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 204 wa kidato cha kwanza hadi cha nne Shule ya Sekondari ya Mwanza Lutheran inayomilikiwa na Kanisa KKKT-DMZV ilianzishwa mwaka 2020 na imefanya vizuri kwenye matokeo ya Kidato cha pili na kidato cha nne kwa Mwaka 2024 na 2025. Uwekaji wa jiwe la msingi umeambatana na zoezi la upandaji miti Katika eneo la Shule ili kuendelea kutunza Mazingira ambapo viongozi wa Dayosisi ,Bodi ya shule na wanafunzi wamepata nafasi ya kupanda miti hiyo.