HUDUMA YA ASKOFU NA WAHUBIRI MORIA LWAMGASA JUNE 2023

Huduma ya Askofu na Wahubiri (ASWA) ina mshukuru Mungu sana kwa matendo makubwa. Jumla ya Wahubiri waliohudumu katika huduma hii ni 320, Wachungaji 43, Wainjilisti 17, ParishWorkers 5 Jumla ya Kaya zilizotembelewa ni 1,315 Jumla ya watu waliofikiwa na kushuhudiwa ni 5,244, watu waliompokea Bwana Yesu Kristo na kuhitaji ubatizo ni 822. Jumla ya watu waliompokea Bwana Yesu katika mkutano ni 246 Watu waliopokelewa kutoka madhehebu mengine ni 63. Wanaume 17 na Wanawake 46 Jumla ya watu waliobatizwa ni 276: Wanaume 27, Wanawake 45, Watoto 204.