DMZV YABARIKI WACHUNGAJI 16

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Dayosisi Mashariki ya ziwa Victoria limewabariki wachungaji 16 wa dayosisi hiyo na kuanza majukumu yao Rasmi katika vituo vya kazi walivyopangiwa . Tukio Hilo limefanyika siku ya jumapili ya September 28, 2025 katika usharika wa Upendo Geita na kuongozwa na Askofu wa DMZV Oscar Itael Lema aliyewabariki wachungaji hao na kuwataka kwenda kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu zaidi kama walivyopata mafunzo kutoka chuoni . Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo msaidizi wa Askofu wa DMZV Dean Stephen Ling'hwa John ,viongozi kutoka ofisi kuu ya Dayosisi ,Halmashauri kuu, Wachungaji wa Sharika zote pamoja na washarika kutoka Geita ,Mwanza na mikoa Jirani