NAFASI YA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elvd.net
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza, Geita na kwingineko.
Uongozi wa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria unatangaza nafasi ya kazi kama ifuatavyo:
1. NAFASI YA KAZI: Mhasibu Msaidizi
IDADI YA NAFASI YA KAZI: Mbili (2)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu KKKT-DMZV
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Fedha KKKT-DMZV
WAJIBU WA MHASIBU MSAIDIZI:
· Kuandaa malipo, statement, nyaraka za kutoa na kupokea fedha kwa usahihi
· Kuhakikisha kuwa malipo yote yanayofanyika yana viambatanisho sahihi na toshelevu
· Kuhesabu bill za wateja
· Kutunza mafaili ya nyaraka za malipo/matumizi na mapato kwa mpangilio mzuri na hali ya usafi
· Kutunza nyaraka za makato ya kisheria kwenye mafaili maalum
· Kusaidia mchakato wa kutengeneza bajeti
· Kuandaa Payment Voucher kwa mujibu wa malipo halali
· Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za Fedha za Dayosisi
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada ya kwanza ya Uhasibu kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali
· Awe Mkristo Mlutheri
· Moyo wa kutumika Kanisani
· Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.
· Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, power point, excel & Accounting Software – Quick Books)
· Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (account preparation & balance sheet)
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja.
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye Sifa Watume/Kuwasilisha Maombi ya kazi kwa:
KATIBU MKUU KKKT-DMZV
S.L.P 423, MWANZA
Kupitia Barua Pepe: elctelvd84@gmail.com
NB: Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Barua Pepe
Muombaji wa Nafsi ya kazi atatakiwa kuwasilisha vitu vifuatavyo:
· Barua ya Maombi ya Kazi,
· Wasifu/CV
· Vivuli vya Vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria (Certified Certificates)
· Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini/Mahali anapo abudu
TAREHE YA TANGAZO: 07/10/2025
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 26/10/2025 SAA: 08:00 Mchana
KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa