Kitengo cha Ukagizi ni kitengo kinachohusika na maswala ya ukaguzi wa sharika, vituo, ofisi za majimbo na ofisi kuu ya Dayosisi kutokana na miongozo ya kanisa (Katiba ya Dayosisi, sera ya fedha, na sera ya ukaguzi ) na miongozo ya nchi ( sera, sheria, na kanuni za nchi). Mpaka sasa kitengo cha ukaguzi kina mtumishi mmoja
Kuwa Dayosisi inayoendeshwa kwa kufuata miongozo na kanuni zilizowekwa katikaDayosisi na nchi ili iweze kufikia malengo yale
- Kukagua sharika, vituo, ofisi za majimbo, na ofisi kuu ya Dayosisi na kuandaa mpango wa ukaguzi wa mwaka
- Kuratibu( kwa kushirikiana na ofisi ya hazina) katika ukaguzi wa nje
- Kufanya vikao vya kamati ya ukaguzi
- Kuhudhuria mafunzo yanayoratibiwa na Bodi ya Taifa ya wahasibu na Wakaguzi wa hesabu
- Kuratibu ajira ya mkaguzi wa ndani
- Kutoa mafunzo na maelekezo kuhusiana na sera ya ukaguzi ya Dayosisi, matumishi yake na mabadiliko yaliyofanyika