Kanisa limesajiliwa RITA, Wizara ya mambo ya ndani na limefanikiwa kuwasilisha marejesho (returns) ya kila mwaka kwa taasisi za usajili za RITA na Wizara ya Mambo ya Ndani. Katiba ya Dayosisi imetafsiriwa kwa lugha ya kingereza. Taratibu za kuchapicha na kuisajili zinasubiri marekebisho ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kamati ya katiba imepokea mapendekezo mbalimbali ya vipengele vya katiba na kupeleka kwenye Mkutano Mkuu kwaajili ya marekebisho
Kuwa dayosisi inayoendeshwa kwa sheria kanuni na taratibu sahihi za dayosisi na nnchi
· Kupokea mapendekezo ya mabadiliko ya katiba, sheria na sera za dayosisi na kuwasilisha kwenye Halmashauri Kuu.
· Kuhakikisha kwamba Dayosisi inatimiza matakwa ya kisheria (annual returns, compliance)
· Kuandaa na kufanya vikao vya pamoja na kamati ya sheria na katiba
· Kutoa mafunzo yanayohusu katiba ya Dayosisi