Kitengo cha Utumishi mpaka sasa kinasimamia jumla ya watumishi 413 wanaume 256 wanawake 157. Kitengo kinaendesha shughuli zake kwa mujibu wa Katiba ya Dayosisi, sera ya utumishi, miongozo mbalimbali na sheria za kazi na za nchi
Kuwa dayosisi yenye watumishi wenye taaluma, ujuzi, ari ya kazi na mifumo imara ya kiutendaji
· Kupokea na kutatua migogoro ya watumishi kazini
· Kuajiri watumishi kwa ngazi zote sharika jimbo, vituo na ofisi kuu
· Kuwajengea uwezo watumishi katika maeneo yao ya kazi
· Kufanya vikao vya watumishi
· Kuratibu na kufanya tathmini ya kazi kwa watumishi
· Kuongeza mishahara na posho za watumishi
· Kuratibu zoezi la Kustaafu kwa watumishi
· Kuandaa na kufanya vikao vya kamati ya Utumishi na sheria za kazi
· Kuwaendeleza watumishi kielimu
· Kutoa mafunzo kwa watumishi yanayohusu taratibu, sheria, sera na miongozi ya kazi (Sharika, Jimbo, Vituo na Mradi)
· Kufanya ukaguzi wa nyaraka, miongozo na taratibu za kuitumishi katika sharika, majimbo, vituo na miradi Dayosisi
· Kuboresha mafao ya ndani ya kustaafu (mkono wa heri)
· Kulipa Mishahara na posho za watumishi