Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kinafanyika kuanzia leo Aprili 29 hadi Aprili 30 katika Ukumbi wa Charming Bungalow-Nyakato. Lengo la kikao hiki ni kupitia taarifa ya fedha januari-disemba 2025 na taarifa ya kazi januari-disemba 2025. Kikao hiki kimeambatana na ziara ya kutembelea na kukagua uzio wa shule ya mwanza lutheran secondary iliopo Sinai-Mabatini ili wajumbe wa halmashauri kuu waweze kuona kazi ya ujenzi inayoendelea.