Baba Askofu Oscar I. Lema wa DMZV leo Machi 16, amefungua Warsha ya wiki mbili katika Ukumbi wa Charming Bungalow kwa wasimuliaji wa hadithi za Biblia kutoka makundi ya lugha za Sukuma,Sumbwa,Kerewe,Kara na Taturu. Warsha hii imehudhuriwa na wajumbe toka LBT(Lutheran Bible Translators) na SIL International. Seed Company ndio wawezeshaji wa warsha hii kuanzia tarehe 16 Machi hadi 27 Machi 2026.