Zaidi ya Wanafunzi 2,000 wamefanya Mtihani wao wa kuhitimu Elimu ya Kipaimara tarehe 05 Septemba, 2026 kupitia vituo 108. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) hutoa Elimu hii ya Imani kwa Watoto/Vijana ili kuimarisha ufahamu wao juu ya Imani yao katika Kristo kwa miaka miwili. KKKT - DMZV Kitengo cha Elimu ya Kikristo kilichopo chini Idara ya Uinjilisti, Misioni na Uwakili usimamia Utoaji wa Elimu ya Kipaimara kupitia Wachungaji, Wainjilisti na Wasaidizi wa Sharika. Idara ya Uinjilisti, Misioni na Uwakili kupitia Kitengo cha Elimu ya Kikristo inawashukuru Wasimamizi wote 114 (Wachungaji na Wainjilisti) chini ya Wakuu wa Majimbo kwa usimamizi wao mzuri wa Mtihani huu uliofanyika.