UWEKAJI JIWE LA MSINGI MTAA WA CARIVARY-NYAFLA

ASKOFU LEMA ASISITIZA UWEKEZAJI KANISANI Askofu wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria DMZV Oscar itael Lema amezitaka sharika zote kujikita kwenye uwekezaji wa miradi mbalimbali kwamaana ili kanisa liweze kupiga hatua ni lazima uwekezaji mkubwa ufanyike hali itakayoisaidia kuanzisha makanisa mengine na Neno la Mungu likahubiriwa kila Mahali. Wito huo umetolewa leo Machi 15, 2026 wakati wa ibada ya uwekaji wa jiwe la msingi Kanisa la KKKT Mtaa wa Carivary-Nyafula uliopo Igombe wilayani Ilemela mkoani Mwanza ambapo Askofu Lema amesema Viongozi wa Sharika wasikubali kuridhika na walicho nacho sasa bali wajikite kuwekeza zaidi kwenye ujenzi wa makanisa pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali itakayosaidia kuongeza mapato yatayosaidia kuinua uchumi wa kanisa na jamii kwa ujumla. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa DMZV Bwana Joshua Kyelekule amezikumbusha Sharika zote kujikita kuwekeza kwenye Ardhi kwani hiyo ndio njia sahihi ya kufanikisha uwekezaji kwani bila Ardhi hawataweza kujenga makanisa pamoja miundombinu ya kijamii kama Shule, pamoja Hospital Naye mchungaji kiongozi wa usharika wa Ebenezer- Pasiansi Mchg. Zakayo Maliganya amewashukuru washarika wa Ebenezer- Pasiansi kwa kujitoa kujenga mtaa huo na kuahidi kuendelea kujenga mitaa zaidi ili kufikisha neno la Mungu kila mahali huku washarika wa Mtaa wa Nyafula wakisema ujenzi wa kanisa hilo utawaletea umoja mshikamo na kuachana na vitendo vya kujihusisha na imani potofu. Askofu Lema na Maidizi wa Askofu Stephen Ling'hwa John wamekuwa na ziara ya Siku mbili katika Usharika wa Ebenezer-Pasiansi ulipo Jimbo la Mwanza Kati ambapo Machi 14 waliweka jiwe la msingi nyumba ya mchungaji na jumapili hii wameweka jiwe la msingi Mtaa Carivary-Nyafula uliojengwa na Usharika huo ambao hadi sasa umegharimu zaidi ya Shilingi Millioni 13