KKKT-DMZV YAUFUNGUA RASMI USHARIKA WA YORDAN NYAHINGI NA KUWA USHARIKA. Askofu wa Dayosisi Mashariki ya ziwa Victoria Oscar itael Lema ameongoza Ibada ya ufunguzi rasmi usharika wa Yordan Nyahingi uliopo Jimbo la mwanza kusini kuwa Moja ya Sharika zilizopo kwenye dayosisi hiyo . Akiufungua usharika huo Askofu lema amewaasa Waumini wa usharika huo wawe tayari kuhudhuria Ibada na kuona umuhimu wa kushiriki ibada kwa utulivu kwamaana wapo baadhi ya waumini hawapendi ibada na kama wakienda ibadani wanataka ibada iende haraka ili waondoke mapema kuendelea na shughuli zao binafsi. Askofu Lema ameongeza kuwa Wakristo wanapaswa kuwa na kiu ya kusikiliza neno la Mungu na kulielewa na kuwa na Roho mtakatifu ndani Yao kwa kuwa ndiye aliye kiongozi Mkuu atakayewafundisha yote yanayowapasa kuenenda na kutenda. Pia Askofu Lema ametoa ujumbe wa neno la Mungu kutoka (Yohana 14:26) {26}"Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia" Usharka wa Yordan nyahingi unaosimamiwa na Mchungaji Emmanuel sitta ulizaliwa kutoka usharika wa Galilaya Buhongwa Mwaka 2013 na mwaka 2015 ukatangazwa kuwa usharika wa mazoezi na mwaka 2021 dayosisi iliuthibitishia kuwa wamekidhi vigezo vya kuwa usharika Kamili na Leo Juni 08 2025 umefunguliwa rasmi ukiwa na jumla ya waumini 410. Ibada ya ufunguzi wa usharika huo imehudhuriwa na mkuu WA Jimbo la Mwanza Kusini Mchunga Daniel Kaijunga ,wachungaji wa Jimbo Hilo ,Viongozi kutoka Ofisi Kuu ya Dayosisi wakiongozwa na katibu mkuu Joshua Petro Kyekule ,wajumbe wa Halmashauri kuu ya DMZV Na Jimbo la Mwanza kusini