UBARIKIO WA WACHUNGAJI 03/09/2023

Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle amewabariki watheolojia watatu (3) kuwa wachungaji rasmi ambao ni Mthe. Emmanuel Lyanga, Mthe. Joshua Mikumo na Mthe. Fredrick Mdiga katika Ibada ya Siku ya Bwana ya 13 Utatu Jumapili tarehe 03/09/2023 katika Kanisa la KKKT-imani Kanisa Kuu. Ibada hii pia imeambatana na kuwaingiza kazini wajumbe teuliwa wa Halmashauri Kuu ya KKKT-DMZV na kuwaaga wajumbe waliomaliza muda wao.