MAHAFALI YA KWANZA YA KIDATO CHA IV MLSS

Mgeni Rasmi Mhe. Baba Askofu Andrew Petro (Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria) amewaomba Jamii nzima na wadau wa Elimu kuendelea kufadhili masomo ya wanafunzi wenye uhitaji na wanaoishi katika mazingira magumu. Ameongea hayo katika sherehe ya mahafali ya kwanza ya kidato cha nne IV katika shule ya Sekondari ya Kilutheri Mwanza iliyofanyika Jumamosi tarehe 26/11/2023. Jumla ya wanafunzi 35 wamehitimu. Idadi ya wavulana 21 na wasichana 14. Pia mgeni rasmi ameahidi kuboresha miundo mbinu ya shule ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa Bwalo na ujenzi wa Bweni la wasichana. Pongezi nyingi za dhati kwa waalimu na wafanyakazi wote wa shule na uongozi kwa ujumla kwa bidii na kujituma kufanikisha hatua hii kubwa.