Watumishi watano kutoka KKKT-DMZV wamehudhuria Mafunzo ya Siku 3 kuanzia tarehe 17 Machi hadi tarehe 19 Machi yaliyoandaliwa na mradi wa Felm. Mafunzo yalihusu uboreshaji wa Mipango na Utekelezaji wa shughuli za kijamii kwa kuzingatia haki za watu wenye mahitaji maalum, usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa wanufaika wa Mradi. Mafunzo haya yalifanyika Arusha katika hotel ya New Safari Hotel