Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, KKKT, limeendesha mafunzo ya siku tatu kwa wakaguzi wa ndani, watunza hazina pamoja na makatibu wa mipango na maendeleo kutoka Dayosisi 29 za kanisa hilo nchini. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha usimamizi wa fedha na rasilimali za kanisa pamoja na kuongeza uwezo wa kupanga na kutekeleza mipango endelevu ya maendeleo. Mafunzo hayo yamefanyika katika Kituo cha Lutheran Junior Seminary mkoani Morogoro.